Aina za miti na sifa zake

Huku Njombe kwenye mashamba yangu ya miti ninaona baadhi ya mashamba ya wenzangu yana miti ya mipaina ambayo ina utofauti na hii ya kwangu, miti hiyo niliyoiona yenyewe haina matawi mengi halafu inanyooka vizuri na inakua haraka, sasa naomba kuuliza kuna aina ngapi za miti hii ya mipaina?
Hivi nikiiona nawezaje kuijua kama ndio aina fulani ya mipaina na inaweza patikana vipi na bei zake?

Nitashukuru sana nikijua mapema ili nione kama nitaweza kununua na kupanda shambani kwangu msimu ujao.

3 Likes

Hongera sana kwa namna unavyojiendeleza na uwekezaji katika sekta ya Misitu.
Kwa upande wangu nakushauri kama unania ya kujifunza zaidi ni vizuri ukatembelea shamba la Miti la Kisonlanza ambalo lipo baada tu ya mji wa Mafinga na kabla ya Ifunda.

Wameanzisha shamba kubwa kwa ajili ya mafunzo na pia wanazo aina tofauti zaidi ya 20 za Miti ya Mipaina na zaidi ya aina 30 za Miti ya Milingoti/Mikaratusi.

Pale kuna aina tofauti za uanzishaji wa mashamba ya Miti ya Mipaina na pia wanaweza kukupatia elimu zaidi juu ya kilimo cha Miti kwa kuzingatia njia bora na matumizi ya mbegu za kisasa kama hizo ambazo umeziona hapo shambani kwako.
Karibu wasiliana na hawa jamaa wanaitwa FDT ndio waaanzilishi wa shamba hilo.

1 Like