Furaha ya Mkulima wa Miti wakati wa Mavuno ni ipi?

Hapa navuna miti yangu ya Mipaina huko Makete kijiji cha Ng’anda.

Naomba kusema neno hapa kwa wadau wenzangu wa MitiBiashara. Nimekuwa Mkulima kutu wa kilimo cha miti kwa miaka kadhaa hadi hivi karibuni nilipo gundua kuwa ile furaha yangu wakati wa mavuno haikuwa yenye ukubwa uliopaswa kwani niliumia baada ya kuona wenzangu wakipata faida zaidi ya mara tatu kwa shamba ambalo ni dogo kuliko hata langu.
Kitu cha msingi ambacho nataka kuwaeleza hapa ni kuhusiana mbinu wakulima wenzangu wa Miti Biashara tunaweza kuzitumia ili kuongeza faida katika mavuno yetu.

Kwanza ni kuzingatia miche yenye ubora kabla ya kuipeleka shambani ili kuhakikisha miti yote inapona na kuwa na afya bora.

Pili ni kuzingatia umbali na palizi angalau kwa mwaka wa kwanza. Hii ni muhimu sana kwani kupanda miti karibu kunafanya isiweze kunenepa vizuri kwani miti inahitaji chakula, hewa na mwanga wa kutosha. Angalau upande kwa spacing ya miguu/mita 3x3 au futi 9x9.

Tatu ni kuhakikisha kila baada ya miaka mitano unapunguzia matawi na idadi ya miti kwenye shamba lako.
Yaani mkulima mwenzangu katika yoote hapa ndio pana umuhimu zaidi kwani kwa muda mrefu nilielewa kuwa na miti mingi shambani ndio hela nyingi. Hili sio kweli hata kidogo na kama yupo anayesema ni kweli aje hapa!
Kwa sasa naweza sema muda huu nakuwa karibu sana na mashamba yangu ili kuhalikisha njia za moto zimetengenezwa na haudhulu shamba na pia kila mti uliopo shambani unafaida.

Yaani kwa sasa ukifika kwenye mashamba yangu hutatamani kuondoka kwani mi mazuri na ninasubili kuvuna hadi 2025 pale miti itakuwa na umli wa miaka 15.

Na ninahakika furaha ya mavuno itakuwa tofauti na kubwa zaidi kwani kwa makadilio kwa heka moja nategemea kupata si chini ya milioni 35TSh.

5 Likes

Kwa Spacing inayoshauriwa; NINA SWALI…
Je nikiamua kupanda milingoti kwa spacing ya 22 halafu baada ya miaka 5 nafanya thinning,
Thinning naifanya kwa kutoa kila mti ulio katikati ya 2
2 (raw and column), then nitazalisha 4*4 nikimaliza thinning yangu…

JE HII SIO TECHNIC BORA YA MANAGEMENT?

2 Likes

Sio 22 ni 2x 2 (spacing)

1 Like

Nifikiri kwa mti wa mlingoti inawezekana ila inatakiwa kuwa makini kuangalia kazi ya ukuaji wa shamba lako.

Kwani kuna sehemu nyingine mlingoti unakuwa kwa kasi sana kufanya hadi mwaka wa tatu tayari miti imerefuka na kufaa kuvunwa, huku ikiwa imefungamana sana.

Kwa upande wangu nashauri spacing ya 2x2 itumike kwenye maeneo ambayo Milingoti ukuaji wake ni taratibu na vizuri kutuma spacing ya 2.5 x 2.5 kwa maeneo ambayo ukuaji wake ni mzuri.

2 Likes

Asante sana kwa darasa @kabago

1 Like