Kurudishia miti iliyokufa shambani

Ni asilimia ngapi ya uponaji wa miti shambani ambayo hainihitaji kurudishia ile iliyokufa?

Habari,
Naomba nikushauri kutokana uzoefu wangu wa ukulima wa miti ni vizuri kurudishia miti miti iliyokufa itazidi asilimia 25. Hivyo ni vizuri kuhakikisha miti iliyopandwa inapona kwa asilimia 75.

Kabago asante kwa ushauri wako sasa shamba langu limepona kwa wastani wa asilimia 40 na mwaka mzima umepita nifanyeje maana nachukia hata kwenda kuliona

Pole sana kwa yaliyokupata katika shamba lako la miti. Kwa kitaalam shamba la miti likipona kwa zaidi ya 80% hakuna ulazima wa kulidishia (wateja rudishia au kama uwezo umepungua waweza kuacha ), likipona kwa 75% ni lazima urudishie. Ikiwa ni chini ya hapo basi lazima upande upya. Ni vizuri wakati wa kupanda ufuate kanuni bora za upandaji na kutumia miche yenye ubora (improved seedlings) na upande wakati kuna unyevu wa kutosha ardhini. Kama ukihitaji maelezo zaidi tafadhali usisite kuuliza kupitia "Ask the Experts "