Kutunza na kuotesha mbegu za mti wa mkaratusi/mlingoti (Eucalyptus)

Kuhifadhi mbegu.

Kuhifadhi mbegu kwa muda mrefu kunahitaji umakini na ufuatiliaji wa karibu zaidi. Mbegu zihifadhiwe katika mahala pakavu na penye ubaridi. Iwapo hali hiyo haitapatikana, mbegu zaweza kuhifadhiwa katika hali ya kawaida mbali na wadudu pamoja na jua. Mbegu zioteshwe kabla ya mwaka mmoja baada ya kukusanywa.
image
Kuzihudumia mbegu kabla ya kuzisia sio lazima ila inahitaji umakinini wa ufatiliaji kutokana na sifa zake na ni vyema kutumia wazoefu kutoka eneo husika.

NB: Muone afisa misitu aliyekaribu na eneo lako kwa usaidizi zaidi.

Kusia mbegu

Muda muafaka wa kumwaga mbegu za mkaratusi/mlingoti ni mwezi Septemba, miezi mitatu kabla ya kuipeleka shambani. Kwa maeneo mengi ambayo wakulima wanaanza kupanda miti mwezi wa kwanza ni vizuri kufuata kalenda hii.

Kiasi cha mbegu kisambazwe katika eneo kuanzia ukubwa wa futi mbili kwa tatu katika kitalu kwa kiasi kidogo cha mbegu. Pia tuta la kusia linaweza kuwa na ukubwa zaidi ya huu kuzingatia wingi wa mbegu ili kutoa nafasi ya angalau sm. 0.5 kati ya mbegu moja hadi nyingine. Mbegu zifukiwe na mchanga kwa kina cha milimita moja ili kuzipa uwezo wa kupata mwanga wa jua, hewa pia kuwezesha kuchomoza kwa urahisi.

Uotaji wa mbegu

Kilo moja ina mbegu za mkaratusi/mlingoti iliyoboresha inaweza kiasi cha miche 300,000. Kwa mbegu zisizoboreshwa ina uwezo wa kutoa miche 100,000. Kwa uotaji huu sawasawa na miche 300 au 100 kwa gramu moja. Kwa kawaida mbegu za mkaratusi zinaanza kuota baada ya wiki moja (Wiki Moja) baada ya kuzisia kwenye kitalu.

Kuhamisha miche

Kuhamisha miche kutoka kitaluni kwenda kwenye viriba kufanyike kati ya wiki mbili au tatu (siku 14-21) baada ya kusia. Tuta la kitalu lazima limwagiwe maji ya kutosha kabla ya kung’oa miche. Umakini ni muhimu sana kwenye hatua hii kwani uzoefu na uzingatiaji wa namna ya kutoa miche kwenye kitalu. Zingatia kushika kwenye majani na sio kwenye kishina chake wakati wa kuhamisha miche midogo. Viliba kwa ukubwa wa nchi TATU ndio zinapendekezwa zaidi kwa miche ya mikaratusi ili kuipa ukuaji mzuri.

Kutunza miche kitaluni.

Miche ya miti ya mkaratusi inatakiwa kutunzwa kwa kupangwa vizuri kwenye kitalu kulingana na ukubwa/urefu pia kumwagiliwa angalau mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni. Pia miche inatakiwa ipangwe kwa nafasi ili kuipatia hewa, mwanga na virutubisho vya kutosha.

Kabla ya kupandwa miche ya mkaratusi hakikisha imefika angalau urefu wa angalau futi MOJA. Kumbuka ni LAZIMA kukatia mizizi siku tano kabla ya kupeleka shambani ili kuikomaza miche ili kuiwezesha kukabiliana na hali mpya ya shambani.
image
KUMBUKA ni hasara zaidi kupanda miche ambayo haija tunzwa vizuri/kitaalam kwenye shamba lako. Miche ambayo haina udongo baada ya kung’olewa kwenye maotea ni rahisi kufa kwani idadi kubwa ya mizizi yake inakuwa imeharibiwa na pia haina uwezo wa kustahimili mazingira mapya kwa urahisi.

2 Likes

Mkaratusi uwa tayari kuvuwa baada ya muda/miaka mingapi?

Nimeambiw pia kwamba kuna mbegu za kisasa,zinapatikana wapi?

1 Like

Mkaratusi/mlingoti unaweza kuvunwa katika umri tofauti tofauti kutokana na matumizi na sehemu ulipopandwa (site quality). Unatakiwa kujiridhisha eneo unalopanda linastawi aina ipi ya mlingoti maana kuna aina zaidi ya 600

  1. Kwa mbao utauvuna kuanzia miaka 12 na kuendelea

  2. Kwa nguzo za umeme utavuna kuanzia miaka 8 na kuendelea

  3. Kwa ajili ya milunda na nguzo za fensi pia umri unapungua

Kwa Nyanda za juu kusini mlingoti aina ya grandis unastawi vizuri sana, lakini pia kuna aina nyingine

1 Like

Pia mbegu za grandis zinapatikana kwa Jambe Agro au kwa wasambazaji kama TFA lakini pia kununua miche moja kwa moja kwenye vitalu vilivyonunua mbegu bora

1 Like