Kuzuia mchwa shambani

Tafadhali naomba msaada.mimi miti yangu inashambuliwa Sana na mchwa,hivyo naomba nifahamu namna ya kuwadhibiti

2 Likes

Karibu sana kwenye forum ya MitiBiashara,

Pole na shida hii ya mchwa kwenye shamba lako.
Kwa kawaida kuna njia kuu tatu za kuzuia na kutoa mchwa shambani.

  1. Kupalilia na kuondoa magugu na mimea mingine kwenye shamba ili kuzuia wasiweze kuishi na kuingia shambani. Yaani hii inahusisha zaidi usafi wa shamba ili kupunguza vichaka.

  2. Kutumia dawa ya kuwaua mchwa. Nenda kwenye duka la pembejeo waambie wakupe dawa ya kuuwa mchwa. Pia unaweza kutumia oil au mafuta kama diesel ila sio petrol kumwaga ndani ya kuchuguu na hakikisha dawa au oil imeingia kwenye shimo lenye mchwa.

  3. Kuchimba na kumtoa malkia wa kundi la mchwa. Hii ni kazi kubwa ila ndio yenye tija katika kuthibiti mchwa shambani. Kwani kwa kumtoa na kumuua malkia itafanya kuuwa kabisa kundi hilo la mchwa.

Karibu sana.

1 Like

Shukran Sana kwa ushauri

Ushauri mzuri sana,

Nafikiri pia unaweza kufanya uchunguzi wa eneo kabla ya kuamua kupanda miti ili kuepuka hasara.