Kwanini tuwekeze kwenye miti biashara?

Kuna fursa iliyopo ya uwekezaji katika sekta ya misitu na msukumo wa ukuaji wake endelevu, unaowahakikishia wakulima wadogo na wakubwa kutumia fursa shindanishi katika biashara ya mbao, nguzo, mirunda na nishati katika kujenga uboreshaji wa uchumi, mazingira, na jamii. Yafuatayo ni mambo MATANO muhimu kuzingatiwa katika uwekezaji katika sekta ya misitu;

 1. Mahitaji ya Miti Kuongezeka.
  Kufikia mwaka wa 2030, mahitaji ya mbao yataongezeka kwa mara mbili ya hali ya sasa na yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku kwa sababu misitu kupungua, maendeleo ya bidhaa za misitu na idadi ya watu inazidi kuongezeka. Hata hivyo hadi sasa mahitaji ya nishati na karatasi bado kwa kiasi kikubwa yanategemea mazao ya miti.

 2. Bei ya Miti Kuongezeka Zaidi.
  Kuadimika kwa mazao ya misitu sokoni kama vile mbao, nguzo, mirunda, kuni na bidhaa nyingine za miti kunapanua fulsa ya biashara na thamani ya uwekezaji katika sekta ya misitu nchini. Mti huongezeka thamani kadri unavyokua “thamani juu ya kisiki” katika kiwango cha zaidi ya mfumuko wa bei. Kwa mujibu wa mwekezaji Jeremy Grantham, bei mbao katika karne iliyopita (~ 1905-2005) thamani ya mazao ya miti imeongezeka kwa kiwango ambacho ni takriban 3% zaidi ya mfumuko wa bei.

 3. Miti Inaweza Kurudisha Faida Zaidi Kuliko Hasara.
  Biashara ya miti inauwezekano wa kulipa zaidi ya kupata hasara(Risk/Return Trade off). Hii inamaanisha biashara hii ina ambatana na hatari kubwa ya kuanguka lakini ikiwa na uwezekano mzuri wa faida kubwa katika kuzingatia maamuzi ya uwekezaji. Hata hivyo misitu ina inaweza kubaki na thamani wakati mwingine hata kama ikiharibiwa na moto au majanga ya asili kama tetemeko la ardhi kwani miti iliyoathilika au kuanguka inaweza kutumika kuchana mbao, kuni au kutengeneza karatasi pia ardhi yake kupandwa miti mingine kwa faida ya baadaye.

 4. Miti Ina Uwiano Chini Katika Madaraja Mengine ya Mali.
  Thamani ya miti shambani inaongezeka siku hadi siku na kuweka tofauti ya soko la uchumi mkubwa kuliko madaraja mengine ya mali/uwekezaji. Pia soko la miti sio rahisi kuathirika kirahisi ukilinganisha na madaraja mengine ya mali, kama vile bidha za maghalani, mali fungani na mali isiyohamishika.

 5. Uwekezaji Katika Ardhi na Thamani Yake.
  Ingawa Ardhi muhimu ya kupanda miti inaweza kukodishwa, lakini wawekezaji wengi wa miti wanapenda kununua Ardhi kama fulsa nyingine ya ewekezaji. Ukuaji wa thamani ya ardhi ni moja ya faida muhimu kwa mwekezaji wa miti kwani upatikanaji wa Ardhi unaendelea kuwa mdogo na mahitaji yake yanakua kwa sababu ya ongezeko la idadi ya watu na maendeleo ya kibiashara kupanuka. Thamani ya Ardhi inatofautiana hasa kulingana na ubora/rutuba nzuri katika ustawishaji wa Miti "matumizi ya juu na bora”. Ndani ya Tanzania kuna fulsa nzuri ya uwekezaji katika maeneo ya nyanda za juu kusini kwa sababu ya upatikanaji wa mvua nyingi na ardhi ya mwinuko wa juu inayostawisha mazao mengi ikiwemo miti ya aina mbalimbali.

5 Likes

Yaani hapa ndio nimepata nguvu ya kuongeza mashamba yangu ya Miti.

Tukutane shambani wadau🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️

3 Likes

Aksante sana Safielmbaga kwa mchango wako mkubwa na mpana juu ya umuhimu wa miti biashara. Ni matumaini yangu mdau yeyote atakayesoma maoni yako atazidi kufunguka juu ya faida zinazoweka bayana fursa iliyopo katika uwekezaji katika kilimo cha miti. Jambo kuu la kuzingatia hapa ni kauli mbiu yetu ya " USIPANDE MITI , LIMA MITI"

3 Likes