Maandalizi ya Kitalu cha miche ya miti - Module 2- Video

Video hii inatoa mafunzo ya namna ya kuanzisha kitalu cha miche ya miti

4 Likes

Hii video nimeipenda, inakufundisha kuandaa kitalu hatua kwa hatua na ubora wake ni mzuri asante sana

3 Likes

Safi kabisa,
FDT mmefanya kazi nzuri ya kutupa elimu ya mambo ya kuandaa mbegu.
Nafikiri nitaitumia video hii kujifunza kuotesha mbegu kwa ajili ya mashamba yangu.

Natarajia kuotesha miti ya mipaina mwakani hivi naweza kuwatika sasa ili nipande angalau mwakani ?

2 Likes

Natafuta module ya tano ya FDT uvunaji wa miti

@Machokodo na @emmanuel.sangalali tunaweza kujua upatikanaji wa moduli ya tano kuhusiana na uvunaji wa miti?

Karibu sana Mr. Kabago kwa muda huu ni kama umechelewa kwani mbegu za miti ya mipaina inachukua karibu miezi sita kuanzia kuota kutunzwa kwenye kitalu hadi kwenda shambani.

Hivyo kama utaotesha sasa na unatazamia kupanda hiyo miche kwenye mwezi wa pili mwakani inawezana ila nitashauri uweze kuotesha hizo mbegu moja kwa moja kwenye viliba(tubes) ili kupunguza ule muda wa kuhamisha miche kutoka kwenye kitalu.

@ROGERS
Tunashukuru kwa ufuatiliaji wa karibu wa mafunzo yetu ya Miti Biashara.
Module ya tano bado ipo kwenye matayarisho hivyo naomba tuvute subira kidogo ila sio muda mrefu itakuwa tayari.

Ila kama utakuwa na maswali kwenye uvunaji unaweza kuuliza mkuu.