Magonjwa ya miti

Wadudu wanaokata miti midogo au matawi ya miti huko Tanga vp kuna mdau yeyote mwenye taarifa ya wadudu hao miongoni mwetu?

3 Likes

Ni kweli kabisa mdau, mwaka huu wa 2018 mwezi wa pili nilisoma chapisho lilioandikwa na Ndugu Paulo Lyimo, Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kuhusu mdudu anayejulikana kwa kitaalam kama Paranaleptes reticulata au Girdling beetle

image

na mdudu huyu hukata kama vile msumeno kwenye tip ya miti michanga kwa kuuzunguka akiwa juu ya mti umbali wa mita mbili hadi tisa na baada ya muda sehemu ya juu ya mti uliopekechwa huanguka na mdudu huyo jike hutumia vumbivumbi na sehemu iliyobakia kama sehemu ya kutagia mayai yake

image

image

2 Likes

Huyu mdudu ni hatari sana. Ningependa kufahamu kuwa toka tatizo hili limebainika mpaka sasa ni hatua gani muhimu zimechukuliwa kudhibiti mdudu huyu na ni athari kiasi gani imes
hatokea. Vilevile mdudu huyu ameonekana sehemu nyingine au ni Tanga tu? Anaathiri mikaratusi (Eucalyptus) tu au hata aina (species) zingine?

Hatari sana yaani hapo mti unaupoteza hivihivi.

Nafikiri huku makete hawajafika maana sijawahi kuona wala kusikia.

Hivi unawezaje kuzuia haha jamaa ?

hawa jamaa wanazuilika kwa kukata miti iliyoathirika na kuichoma moto maana ndiyo sehemu ambazo wanatumia kuzaliana

Nimefikiria mbali kidogo kuhusu njia ya kuwazuia au kuwadhibiti hawa wadudu hatari kwa miti aina us mikaratusi. Ukikata miti iliyoathirika na kuichoma bila kushughulika na wadudu wenyewe naona kuna hatari ya wadudu hawa kuhamia katika miti mingine au eneo jingine na kuendelea kuleta madhara. Nimejiuliza kuwa wanapoonekana eneo fulani ni lazima wametoka eneo jingine ndio wakahamia hapo. Kwa mantiki hii (kama INA mashiko ) IPO haja ya kufikiria namna ya kupambana na waduu wenyewe halafu kuharibu mazalio yao. Hapa tunaweza kufikiria kipi kianze, kuharibu mazalia yao kwanza au kupambana na wadudu kwanza ndipo mazalio yafuatie. Bado nakuna kichwa! Mjadala huu bado kwangu ni kitendawili. Nisaidieni kukitegua.

Kumbe na miti yetu ina maadui wakubwa hivi?

Hawa wadudu nikiwakuta shambani kwangu nawakaanga na kuwala na ugali, hawawezi tusababishia hasara kwenye miti mikubwa kiasi hiki.

Nashukuru Mungu huku kwetu njombe sijawaona.

2 Likes

Yaani unataka wawe kitoweo?

1 Like

Naona angalau nitapunguza hasira ya kula miti yangu.