Matumizi ya miti aina ya milingoti

Naomba kufahamishwa kama kuna matumizi mengine yatokanayo na miti ya milingoti mbali na nguzo za umeme.
Pia kama kuna matumizi mengine, masoko yake yako wapi? maana huku kwetu sioni matumizi mengine zaidi ya nguzo.

2 Likes

Ndio kuna matumizi mengi kwa miti ya Milingoti mbali na kuzalisha nguzo za umeme na kama sijakosea mlingoti ndio mti pandwa wenye kutoa mazao mengi zaidi ya miti mingine.

Kwa haraka milingoti inatumika katika kutengeneza mbao za kupaulia pamoja na fenicha, nguzo ndogo za mirunda na fensi, mbao pana za kujengea madaraja, dawaza meno, kuni za kutoa nishati kwenye viwanda, kutengeneza plywood na karatasi.

Kwa matumizi haya miti ya milingoti iko vizuri sana kwenye soko lake na kwa sasa viwanda vingi vipo Mafinga iringa ambavyo vina nunua kwa wingi magogo ya miti hii.