Mbegu bora za miti zinapatikanaje?

Mbegu bora za miti zinapatikana kwa njia ifuatayo:

  1. Wataalam wa kuzalisha mbegu za miti (Tree genetists) huchagua miti bora yenye sifa zinazohitajika (Plus trees) kwa ajili ya kuzalisha zao husika la mti mfano mti ulionyooka kwa ajili ya nguzo/mbao
  2. Kwa sababu tayari “plus trees” huwa ni miti mikubwa/yenye umri mkubwa, tree genetists huchukuwa vikonyo vilivyo katika sehemu ya juu ya miti hiyo na kuvipandikiza (grafting) katika vishina (root stock) za aina ile ile ya mti (same species)
  3. Baada ya upandikizaji, miche hiyo hutunzwa kwa uangalizi mkubwa na kisha hupandwa kwenye shamba la kuzalisha mbegu (Seed orchard)
  4. Shamba la mbegu hutengwa na jamii zinazofanana ili kuepusha mwingiliano wa poleni wakati wa uchavushaji (Controlled pollination)
  5. Wataalam wa uzalishaji mbegu huendelea kufanyia majaribio mbegu zinazopatikana katika shamba na kuendelea kufanya uboreshaji zaidi na hivyo kuwa na vizazi kadhaa vya mbegu bora B
  6. Mbegu bora huwa na sifa kama vile: ukuaji wa haraka, kuzalisha zao lenye ubora, unyoofu, kustahimili magonjwa na wadudu wahalibifu n.k
2 Likes

kumbe hizi mbegu tunazotumia sio bora!
Hivi hizi mbegu bora za miti kwa sasa zinazalishwa hapa Tanzania au?
Na kama zipo zinazalishwa maeneo gani?

Bado najiuliza hivi kwa sisi wakulima wa kawaida huwa tunakosea pale tunapopada miti kwa kutumia mbegu hizi za kawaida ua?

1 Like