Miti ya kisasa ubora wake na changamoto

Hii miti ya kisasa haswa mlingoti, inatatizo kidogo huwa ikifika umri fulani huwa inavunjika vichwa sasa sijui mnatusaidiaje wakulima, tunaipenda inakua haraka sana na ina afya nzuri tatizo ndio hilo kukiwa na upepo mkali inavunjika.

2 Likes

Ni jambo zuri kuwa umegundua faida za miti ya kisasa. Kwa utafiti ambao tumeufanya kupitia miti hii ya kisasa unaonyesha kuwepo na hili tatizo LAKINI ni kwa kiasi kidogo sana, na tatizo hili hasa hujitokeza kwenye maeneo yenye upepo mkali unaoambatana na baridi kali.

Hivyo tunashauri kupanda miti ya kuzuia upepo kwenye mashamba yanayoadhilika na tatizo kama lako. Pia tunasisitiza kuwaona wataalamu kwa ufafanuzi zaidi ili usiweze kupata madhala makubwa.

2 Likes

Naona kwa upande wangu naona hii Miti inafaida zaidi kuliko hasara kwani kwa kutumia hizi mbegu bora miti yangu naona inakuwa kwa kasi zaidi ya ile miti iliyotokana na mbegu za kawaida.

Hivyo nawashauri kuhakikisha tunatumia mbegu za kisasa pamoja na kufuata maandalizi yote kwenye upandaji wa Miti.

1 Like

Mie naomba kuuliza, nitumie dawa gani kwenye miche yangu (milingoti) kitaluni inashambuliwa na wadudu sana.

2 Likes

Kwa hili nafikiri inategemea na aina ya wadudu wanaoshambulia hiyo miche maana kuna aina nyingi za dawa za kuulia wadudu.

Ila kama miche ni midogo sana unaweza kuifunika kwa chandarua ili wadudu wasiweze kufika kirahisi na pia itasaidia kuwezesha kuepusha madhala ya sumu au kemikali za dawa hizo.