Miti ya Mikaratusi/Milingoti

Kwa kutumia mbegu za kisasa Miti hukua kwa haraka na kufanana kimo na unene mkubwa.

Shamba zuri sana, hivi linaweza kuwa na miaka mingapi?

Napenda na langu lifanane kama hili ili nipate faida zaidi nafikiri nitaweza hata kwa hekali kumi tu kujaribu hivi.

Shamba hili lina miaka minne. Kabla ya kupanda shamba liliandaliwa kwa kulimwa kwa tractor na kupandwa kitaalam. Alama ambapo mashimo yalichimbwa ziliwekwa kwa umbali wa 3mx3m na mashimo yalichimbwa urefu wa 30cmx30cm. Baada ya kupanda mbolea ya NPK kiasi cha 30g kiliwekwa katika kila mti ili kuhakikisha rutuba ya kutosha. Palizi ilifanyika mara kwa mara kuhakikisha miti haisongwi na magugu yanayoweza kunyang’anya rutuba. Utunzaji huu ndio umesababisha matokeo mazuri ya ukuaji wa miti katika shamba hili kama unavyoona. Nakushauri fuata ushauri wa matumizi ya mbegu bora, njia sahihi za uanzishwaji wa shamba la miti, upandaji na uhudumiaji sahihi wa shamba hakika utafanikiwa. Usisite kuuliza wataalam pale unapoona huelewi jambo lolote kuhusu shamba la miti.

1 Like

Sahihisho. Umbali kati ya alama moja na nyingine ni 3m kwa 3m na mashimo ni kina 30cm na upana 30cm

Nashukuru kwa ufafanuzi mzuri.

1 Like

Nimependa sana namna hili shamba lilivyostawi. Nashukuru kwa ushauri uliotoa. Tuko pamoja.

1 Like