Mpangilio wa bustani ya miche ya miti

1 Like

Mdau kuna umuhimu gani wa kuzingatia uelekeo wa upepo au jua ninapoweka kitalu changu?

2 Likes

Asante sana kwa swali lako. Uelekeo wa upepe na jua katika dhana nzima ya uchaguzi wa eneo sahihi la kuweka kitalu ni jambo muhimu sana. Upepo unapovuma kupita kwenye kitalu (prevailing wind) unachukua unyevunyevu kwenye miche na kuchangia kwa kiasi kikubwa miche kukosa unyevu na inaweza kuathirika.

Vilevile jua linapopiga moja kwa moja toka asubuhi mpaka jioni (direct sunshine) huchangia kwa kiasi kikubwa miche kukauka. Kama mambo haya mawili yasipozingatiwa, kazi ya umwagiliaji itakuwa ngumu kwani mara nyingi miche itakuwa katika hatari ya kukauka. Ni vema kuzungushia wigo kupunguza upepo na kuepuka kuweka kitalu mahali ambapo jua linapiga moja kwa moja tangu asubuhi mpaka jioni.

2 Likes

Kuna tofauti yeyote ktk kuanzisha kitalu cha mipaina na milingoti?

1 Like