Nina swali kuhusu shamba

Shamba langu lipo mtwango kijiji cha uwelela, na lina udongo wa kukauka na mchwa wengi nimewahi kupanda miti inakufa mara nyingi, baada ya kusikia mbegu bora nikaona niulize kama itaweza kuota kwenye shamba hilo na nifanye nini isife ?

2 Likes

Inashauriwa miti ipandwe sehemu yenye unyenyevu (ardhi isiyo kavu).

Kwa maana ardhi iliyo kavu ndio huvutia mchwa sanaa…

Kwa shamba lako nakushauri uwe unatumia dawa ya kuulia mchwa ili kuokoa miti yako.

4 Likes

Pole sana mdau

Nafikiri ni vizuri kutafuta dawa au namna ya kuwaondoa hao mchwa kwanza ili uwe na uhakika na mazao utakayoyapanda.

Kwa uzoefu angalau mipaina ndio huweza kusyahomili mchwa kuliko milingoti ila kwa hili la mbegu za kisasa naona hakuna tofauti sana kwenye kushambuliwa na mchwa.

1 Like

pole mdau, kama shamba lina vichuguu unaweza kuvivimba ili kumtafuta malkia wa kundi hilo la mchwa ila kama ni vigumu inashauriwa kutumia dawa ya kuulia mchwa inayoitwa nafikiri ni ATTAKAN inauzwa maduka ya pembejeo za kilimo itakusaidia kuweka katika shamba lako ila hata kama ni mbegu bora zitaliwa tu na mchwa mdau

2 Likes