Ninatamani kuwekeza kwenye kilimo cha miti, nianzie wapi?

Habari wana jamvi, hii sekta ya misitu na miti imekuwa ikisemwa kama ni fursa nzuri sana ya uwekezaji na kuongeza uchumi, binafsi mim ni mgeni kabisa sijui A wala B kuhusu miti lakini niko interested kujua kwa undani kuhusu kilimo chenyewe na biashara nzima ya miti.

Kwa wageni kama mimi, natakiwa nianzie wapi?

6 Likes

Karibu sana Stebby,

Kwa upande wangu nami nilianza kwa kujiuliza maswali kama yako na nilihakikisha maswali yote nayatafutia majibu kabla sijaanza kilimo cha miti kibiashara.

Kwa haraka nilikuwa najiuliza ni aina gani ya Miti instawi kwenye eneo langu la shamba, pili nilijiuliza ni wapi napata elimu juu ya upandaji na utunzaji wa Miti Biashara, tatu nilijiuliza je kuna changamoto gani na soko lake liko vipi?

Kwa uzoefu wangu naweza kukushauri yafuatayo;

  1. Kama unamawazo hayo na unategemea kupanda miti kwenye maeneo ya nyanda za juu kusini nakushauri upande Miti ya Mipaina au Milingoti kwani ndio Miti ya biashara inayostawi vizuri zaidi na ina soko zuri ndani na nje ya nchi.

  2. Naomba kukushauri upate elimu juu ya kilimo cha Miti kabla ya kupanda na elimu hii unaweza kuipata kutoka kwa mabwana Miti kotika eneo ulipo au kwenye mitandao kama humu. Ni muhimu sana kupata elimu juu ya upandaji wa Miti kabla ya kupanda ili kuwezeshe kupanga bajeti na kuweza kuwasimamia vizuri watendaji kwenye shamba lako.

  3. Kitu cha muhimu ni kuwa na msimamizi/usimamizi unaoweza kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza kwenye Kilimo cha Miti, hili litasaidia kupunguza hasara. Kulifahamu soko ni jambo la muhimu sana kwenye Kilimo cha Miti Biashara kwani ndio sehemu muhimu ambayo itakuwezesha kuweza KUTENGENEZA faida au hasara kwenye kilimo cha Miti.

Karibu sana mkuu.
#MitiBiashara inalipa.

2 Likes

Asante sana @kabago kwa maelezo mazuri. Nadhani pia ukiwa na muda unaweza kutuandikia wadau maelezo kidogo kuhusu elimu ya upandaji ili tuzidi kujifunza zaidi

3 Likes

Hakuna shida nitajitahidi.

4 Likes

Huku Wilaya Kilolo maandalizi ya kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo cha msimu huu YAMEANZA japo kidogoo tumewahi (maana wengi huanza nwezi wa 09 au 10)…
““INFORMATION IS POWER”” Nakushauri funga safari uje kujifunza kwa macho na vitendo ILI UPATE ELIMU UKIWA FIELD ZAIDI.
Ila pia waweza kuanza na theory ukitumia simu yako na baadae ukaja kujifunza kwa vitendo.

Mi ilinichukua safari ya kutoka Dar kuja kuishi kilolo (kijiji cha kilolo) siku kadhaa kuja kujifunza baadae nikapata fursa ya kukutana na FDT ambao walinifundisha kitaalamu zaidi na UTAALAMU WAO NDIO NINAOUTUMIA MWAKA HUU WA KILIMO 2018/2019.
NA MUDA HUU TUPO SHAMBANI TUKIANZA MAANDALIZI.

1 Like

@kabago asante sana mkuu.

@ALfayo_Jr, safi sana itabidi nitenge muda kutembelea field kuona. FDT nimewapata tayari tumefanya maongezi mazuri sana.

4 Likes

Niliwahi kusikia kuwa serikali imepiga marufuku uagizaji wa nguzo za umeme na pia kulikuwa na kiwanda cha kutengeneza nguzo za zege vipi haya mambo yako vipi wadau?

2 Likes

Ni kweli mwaka 2017, serikali kupitia waziri wa nishati alipiga marufuku uagizaji wa nguzo za umeme kutoka nje especially kwenye mradi wa REA, kuna kiwanda nadhani kipo Iringa kinazalisha nguzo za miti na kingine kipo Bagamoyo kinazalisha nguzo za zege(Sijui hizi za zege zinatumika wapi).

Sifahamu kwa uhakika kama kiwanda cha Iringa kinanunua miti kutoka kwa wakulima au wanavuna kutoka kwenye mashamba yao, nadhani wataalamu wanaoelewa huu mchakato watatupa maelezo zaidi.

2 Likes

Karibu sana kwenye kilimo chenye tija, ushauri wa bure kwako @Stebby ujanja ni kuanzia shambani tu hakuna namna, maana tukiwa huku mjini tunapeana moyo sana kuhusu kilimo cha miti.

Na wakati mwingine tunadanganyana kuwa kilimo hakilipi wakti huo kuna wadau wanapiga hela zakutosha kwenye miti hiyo hiyo.

Kwasasa huku mjini watu wanakisifia sana kilimo cha parachichi wakati hata shambani hawajawahi fika.

Mdau kuhusu nguzo za zege ni kweli hicho kiwanda kipo lakini tusisahau kuwa changamoto kubwa ya nguzo za zege ni katika usafirishaji wake. Unaweza kuwa na nguzo mia lakini kutokana na miundombinu ya kuzifikisha hasa maeneo ya vijijini ikawa shida na ukajikuta uafikisha nusu tu ya mzigo uliobeba

2 Likes

Viwanda vingi vya nguzo ni vya watu ambao hawana mashamba yao na wanategemea zitoke kwenye mashamba ya wakulima hasa wale wa kati na wadogo wadogo. Mfano kampuni la New Forest miti yao haijafikia kuvunwa hivyo ni soko kwa wakulima kama sisi

2 Likes