Plywood kama fursa mpya kwa wakulima wa miti

plywood

Ni jambo la faraja sana kwa mkulima wa MITI kusikia kuwa miti ya mikaratusi/milingoti inahitajika kwa ajili ya kutengenezea plywood. Uhitaji wa mti wa mkaratusi ni mkubwa sana kwa sasa katika viwanda Gina kwa ajili ya kutengenezea plywood. Wilayani Mufindi/Mafinga tayari kuna viwanda vinavyochakata mikaratusi ili kutengeneza plywood.

Miti ya mikaratusi yenye umri unaoanzia miaka mitano humenywa katika mashine maalumu na kutoa veneer ambazo huunganishwa katika kutengeneza plywood. Inaelezwa kuwa bado upo uhitaji mkubwa wa plywood duniani. Hii inatuhakikishia uhitaji mkubwa wa mikaratusi/milingoti kama raw material katika viwanda hivi.

Jambo la msingi ni kuzalisha miti yenye ubora wa hali ya juu utakaowezesha miti kununulika.

4 Likes

Asante sana mdau kwa taarifa hizi nzuri na zenye matumaini kwa sisi wakulima wa miti.

Kwa sababu fulsa ndio imekuja ila kwa sisi amabao tumesahzoea kuuza milingoti kama nguzo, kuni au mbao, unaweza kutusaidia vipimo na namna tunavyoweza kupata nafasi ya kuingiza mzigo kweye hilo soko?

1 Like

Ni miti ya milingoti peke yake ndo inayofaa au ni aina zote za miti mdau?

1 Like

@Mitimingi
Aina nyingi za Miti inafaa kwa kutengeneza plywood hasa migrivelia, mipaina, micyprus na mingine. Ila kwa sasa wadau wengi wanapenda kutumia milingoti kwa sababu inatoa faida zaidi.

Faida ya mlingoti kwenye kutengeneza plywood ni kwamba vipande vinavyobaki baada ya kukata nguzo, mbao au kuni vinaweza kutumika kwa kazi hii.

Kwa maana nyingine miti ya mipaina na micyplus inaweza kutoa mazao ya mbao kwa faida kubwa zaidi hivyo wadau kuweza kuchagua zao la mbao kuliko plywood.

1 Like

Ila nasikia bei wanayotoa kwenye magogo ni ya chini sana

1 Like

Wadau naomba kujua kama nikilima miti kwa ajili ya veneer na ile ya mbao ipi ambayo itanilipa ndani ya muda mfupi kwa ekari moja?

1 Like

Wadau hivi Njombe kuna kiwanda cha plywood na ni wapi kilipo kama kipo