Tangazo la Huduma za Miti, vipi kuhusu bei?

Nashukuru kufahamu sasa naweza kupata huduma hii kirahisi.

Kwa sisi tunaoishi mbali na maeneo ya mashamba naona tutaweza kufaidika sana.
kwa upande wangu ningeomba kufahamu bei za huduma hizo ili iwe rahisi kujipanga.

Hasa kwa hii miche ya kisasa naitamani sana.

3 Likes

Hili nafikiri linahitaji ufafanuzi mzuri ili kuwa na uelewa wa kutosha kwa wadau, au @Pamera unasemaje?

Sifael umeuliza swali la msingi sana hata mimi natamani kujua gharama maana sekta ya misitu haina watoa huduma wengi hivyo tunajikuta tunapata taabu sana tunapohitaji hata ushauri wa kitaalam