Umuhimu wa madalali

Wakulima wengi wa miti wanawategemea madalali wakati wa kuuza miti katika mashamba yao. Je, kuna faida gani au hasara gani kwa mkulima katika kuwatumia madalali?

2 Likes

Madalali wana umuhimu kwa wakulima ambao hawataki kuhangaika kujua bei ya mazao yao sokoni kwa sababu wanawajua wanunuzi hivyo kumpunguzia muuzaji kazi ya kutafuta mnunuzi japo wanachangamoto zao

2 Likes

Aksante Mitimingi kwa mchango wako, lakini kama ulivyokwisha sema kuwa madalali wana changamoto nyingi. Ningependa kujua zaidi hizi changamoto kama zina manufaa gani au hasara gani kwa mkulima wa miti.

1 Like

Madalali ni watu kati, wananunua miti kwa mkulima kwa bei ya chini kabisa kwa sababu tu mkulima ana shida au hajua atapata wapi taarifa za soko. Kuna msemo unasema wa kiingereza unasema “information is power” na kwa sababu Dalali anakuwa na taarifa za wapi anaweza mnunuzi na kwa bei gani ndiyo maana anaweza kufanya biashara zake. Mkulima angekuwa na taarifa za bei ya sokoni angalau ingemsaidia hata katika kukadiria bei ya mazao yake lakini ndiyo wamekuwa wahanga wakubwa

1 Like

Madalali ni watu wabaya sana, walisha wahi kunidhulumu fedha nyingi sana kwenye mauzo yangu ya miti na kunisababishia hasara.

Hadi sasa nimeamua kuuza kwa mteja moja kwa moja tu ili kuepuka sarakasi zao ingawa inachukua muda mrefu ila inanibidi kufanya hivyo.

Hebu nipe ujanja ulioutumia kumpata mteja maana mimi nahisi huwa nagawana jasho langu na hawa Madalali

1 Like

Mbona rahisi sana.

We panda shamba lako kwa miche bora na kuitunza vizuri baada ya miaka kumi wateja wenyewe wataanza kuulizia bei.

Na ukiona hakuna wateja wanaoulizia shamba lako ujue hakuna mali humo.

Ila wadau mi naona madalali bado wana nafasi kubwa katika kuwaunganisha wateja na wakulima, changamoto ni pale uelewa wa mkulima kuhusu hali ya soko ili aweze kutetea bei yake anayouza miti